HabariNewsSiasa

Kitengo cha juu cha usalama nchini Kenya kimewahakikishia raia usalama.

Kitengo cha juu cha usalama nchini Kenya kimewahakikishia raia usalama kufuatia hofu ya kuwepo kwa ghasia zinazohusiana na uchaguzi.

Mamlaka imewataka Wakenya kuanza tena shughuli zao za kibiashara wakisema nchi iko salama na usalama umeimarishwa katika kipindi hiki.

Wingu la wasiwasi limetanda nchini kufuatia machafuko yaliyotangulia baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais Jumatatu.

Kamati ya ushauri ya usalama wa taifa nchini imechukua hatua ya kuondoa hofu ya kutokea ghasia kufuatia mzozo wa matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Timu hiyo ilisema hali ya usalama nchini iko shwari baada ya tathmini ya awali mapema Jumanne na mamlaka imechukua hatua kuhakikisha nchi iko salama.

Kulikuwa na ripoti za ghasia katika maeneo ya mji mkuu Nairobi na katika mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya baada ya waandamanaji kupinga kuthibitishwa kwa William Ruto kama mshindi wa uchaguzi wa Agosti 9.

BY EDITORIAL DESK