HabariNewsSiasa

Rais mteule William Ruto na naibu wake mteule Rigathi Gachagua wamewahutubia viongozi waliochaguliwa katika muungano wa Kenya- Kwanza.

Akizungumza eneo la Karen jijini Nairobi, Ruto amesema kuwa uongozi wake utaruhusu asasi za utawala kuwa huru bila ya kuwatia uwoga watumishi wa serikali.

Amesisitiza kuwa chini ya uongozi wake atatoa nafasi ya kuwasikiliza wakosoaji wa serikali bila vikwazo vya kutishia uhuru wa upinzani.

Aidha ameongeza kuwa hakuna afisa wa utawala ataruhusiwa kushiriki siasa jinsi ilivyoshuhudiwa wakati wa rais anayeondoka rais Uhuru Kenyatta.

BY EDITORIAL DESK