HabariNews

Shirika La Umeme Kenya Power la laumiwa Kaunti ya Kwale.

Shirika la huduma za umeme Kenya Power limetajwa kuchangia katika kudorora kwa biashara za wawekezaji katika kaunti ya kwale.
Akizungumza huko Diani Mwenyekiti wa wawekezaji kwale commerce chambers Salim Mwayogwe almaaruf Zamunda amedokeza kuwa wawekezaji wengi kwale wamelitaja shirika hilo kuwa mmoja ya changamoto kwa wafanyibiashara hao akisema kuwa imewapelekea kukadiria hasara kufuatia ukosefu wa umeme mara kwa mara.
insert….Mwayogwe changamoto
Aidha ameongeza kusema kuwa ipo haja ya serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya kwale kuweka mikakati na mipangilio mizuri kwa kueka sheria madhubuti ya mijengo ili kuweza kuimarisha miji ya manuspaa ili kuweza kuepusha wakaazi kujijengea pasi na mipangilio kabambe ambayo pia inaathiri sana uekezaji katika kaunti hiyo.