HabariMombasaNewsSiasa

Abdulswamad Sharif nassir na naibu wake Francis Thoya wameapishwa rasmi.

Abdulswamad Sharif nassir na naibu wake Francis Thoya wameapishwa rasmi kama gavana na naibu wa pili wa Kaunti ya Mombasa katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa mamangina water Front.

Wawili Hao wamelishwa kiapo mbele ya jaji George Ndulu

Katika hafla hiyo gavana anayeondoka Ali hassan Joho ameeleza matumaini yake kwa uongozi wa gavana Abdhulswamad akisema Mombasa iko salama.

Joho amesema kamwe hataingilia kwa namna yeyote uongozi wa Abdhulswamad na watasalia kama marafiki.

Joho vile vile amedokeza kuwa msimu wa siasa umekwisha na hajutii kusalia katika upinzani, japo anajiandaa na maswala ya siku zijazo.

Kuhusu maswala ya kurejeshwa kwa huduma za bandari na serikali ya William Ruto, Joho amesema wanafuatilia swala hilo kwa makini ili kuhakikisha linatekelezwa.

BY EDITORIAL DESK