HabariNews

Wakaazi wa garsen kaunti ndogo ya tana delta wanatarajia kapata suluhu ya uhaba wa maji.

Wakaazi wa garsen kaunti ndogo ya tana delta huenda wanatarajia kapata suluhu ya uhaba wa maji vijijini iwapo maafisa wanaohusika na ukarabati wa mitambo ya kusambaza maji watafanikiwa kutatua hitilafu hiyo inayokumba mitambo hiyo.

Kaimu mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji maji kaunti ya Tana River TAWASCO, William Jilloh amesema changamoto hiyo ya maji imetokana na kisima cha Idsowe kinachotumiwa kusamabaza maji maeneo ya Garsen kuingia matope hali iliyochangia bomba la kusambaza maji kuungua.

Amehakikishia wakazi kwamba tayari vifaa vimenunuliwa ili kufanyia ukarabati bomba hilo.

Aidha amesema TAWASCO inapania kukarabati kisima kilichoko maeneo ya feri ya zamani mjini Garsen ili kusambaza maji na kukidhi mahitaji ya ongezeko la watu.

Wakati huo huo Jilloh amethibisha kwamba deni linalodawa kampuni ya TAWASCO na shirika la kusambaza umeme nchini KPLC limelipwa baada ya KPL kusitisha huduma zake mwezi uliopita kutokana na malimbikizi ya deni na kusababisha uhaba mkubwa wa maji Tana River.

BY EDITORIAL DESK