HabariMombasaNews

WAHUDUMU WA BODABODA, TUK TUK NA TEKSI KAUNTI YA MOMBASA WAKONGAMANA KUZINDUA MUUNGANO WA KUWASILISHA MATAKWA YAO.

Wahudumu wa bodaboda, tuk tuk na teksi kaunti ya Mombasa wamekongamana katika hafla ya kuzindua muungano wa kuwasilisha matakwa yao.

Wakizungumza na vyombo vya habari wachukuzi hao wameeleza kuwa usalama kwa abiria wanaosafiri usiku na ada za juu ni baadhi ya masuala ambayo muungano huu unalenga kujadili na kuhakikisha kuwa sekta ya uchukuzi kaunti ya Mombasa imeboreka ili abiria wazidi kufurahia huduma zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Tuk Tuk kaunti ya Mombasa Benjamin ochwango amesema kuwa muungano huo utatoa mafuzo ya nidhamu miongoni mwa wachukuzi na pia kuwaelimisha kuhusu jinsi ya kutatua visa mbalimbali vitakavyotokea katika shughuli zao za kila siku.

BY EDITORIAL DESK