HabariNews

Rais William Ruto amesema kenya iko tayari kununua mafuta kutoka taifa la urusi.

Katika mahojiano na shirika la habari la BBC, Ruto amesema jukumu lake kama rais ni kukuza uhusiano wa kenya na mataifa mengine kama vile urusi.

Ruto amesema hatua hiyo inalenga kukabili bei za mafuta ili kuboresha uchumi wa taifa.

Mataifa mengine ulimwenguni yameendelea kujitenga na urusi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.

Licha ya kupanda kwa bei za mafuta Ruto ametetea uamuzi wa serikali wiki jana kuondoa ruzuku katika bidhaa na kuelekeza katika uzalishaji akisema ilikuwa inawafaidi wachache mno.

Kenya inakumbwa na mgogoro wa kiuchumi hali ambayo imechangia bei za mafuta na vyakula kuongezeka hat ana zaidi.

BY EDITORIAL TEAM