FoodHabariNews

Kaunti ya kwale ni miongoni mwa kaunti 23 nchini zitakazopokea chakula cha msaada.

Kaunti ya kwale ni miongoni mwa kaunti 23 nchini zitakazopokea chakula cha msaada kutoka kwa serikali ya kitaifa hii ni kutokana na baadhi ya maeneo kuathirika na ukame .

Hapa kaunti ya Kwale baadhi ya sehemu za Kinango na Lungalunga ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika na kiangazi kwa muda mrefu.

Gavana Fatuma Achani amesema kuwa mbali na serikali kuu kutoa chakula cha msaada kwa wananchi serikali yake aidha itawekeza zaidi katika uchimbaji wa mabwawa zaidi ya maji ili kukabiliana na changamoto ya maji inayoshuhudiwa hususan nyakati za kiangazi.

Achani vile vile ametahadharisha wanaolenga kuuza chakula cha msaada kuwa serikali itawakabili vilivyo

Wakati huo huo gavana Achani amehimiza wakaazi kuripoti visa vya utepetevu miongoni mwa wahudumu wa afya katika kaunti hiyo.

Achani anasema hatua hiyo inalenga kukabiliana vilivyo na changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye hospitali na zahanati za umma katika kaunti hiyo.

BY EDITORIAL TEAM.