HabariMazingiraNews

Mabadiliko ya hali ya anga yapelekea mzozo baina ya wanyama pori na binadamu.

Mzozo baina ya wanyama pori na binadamu ni kutokana na mabadiliko ya hali ya anga.

Kulingana na msimamizi wa shirika la kuhifadhi wanyama pori tawi la Kwale KWS, Jacob Orahle amesema kutokana na kiangazi kinacho shuhudiwa kwa sasa katika baadhi ya sehemu hapa kaunti ya Kwale wanyama hao huvuka ua wao kwa kutafuta maji ya kunywa ikizingatiwa kwamba vyanzo vingi vya maji vimeweza kukauka kutokana na hali ukame iliko kwa sasa.

Aidha afisaa huyo ameendelea kusema kuwa kukatwa miti ya makaa na kuwindwa kwa wanyama hao kumesababisha wanyama kuhangaika kutokana na kuharibiwa kwa makaazi yao.

BY EDITORIAL DESK