HabariMazingiraNews

Watu wawili waendelea kuuguza majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na chui Kwale.

Watu wawili waendelea kuuguza majeraha mabaya katika hospitali ya Samburu baada ya kushambuliwa na chui katika kijiji cha Batani huko samburu kaunti ya Kwale.

Naibu kamanda wa polisi eneo la Samburu Fredrick Ombaka amethibitisha tukio hilo akisema kwamba kutokana na ukame unaoshuhudiwa Chui huyo alivamia kijiji hicho baada ya kutoroka mbugani Tsavo amemjeruhi Willy Chirima Bembeyu mwenye umri wa miaka 52 na Tsuma Lalo mwenye umri wa miaka 19 waliokuwa katika shughuli zao za siku kabla ya chui huyo kuuwawa na wanakijiji.

Hata hivyo shirika la wanyamapori KWS Kwale limethibitisha ongezeko la wanyamapori kurandaranda mitaani kufuatia makali ya kiangazi mbugani, ikiwataka wakaazi kuwa waangalifu kwa usalama wao.

BY EDITORIAL DESK