HabariNewsSiasa

Rais William Ruto amehakikishia baraza lake la mawaziri ushirikiano wa dhati wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi baada ya mawaziri hao kulishwa kiapo, rais Ruto amesema ushirikiano huo ndio utakaofanikisha ajenda ya maendelea kwa wananchi.

Ruto vile vile ametoa changamoto kwa mawaziri hao kuhakikisha wanatekeleza na kuiheshimu katiba ya nchi katika majukumu yao.

Wakati huo huo Kiongozi wa taifa amekumbusha mawaziri hao kujitenga na maswala yatakayoleta tashwishi katika uongozi wao na kuhakikisha wanahudumui kila mmkenya.

Baraza hilo limeongozwa na mkuu wa mawaziri musalia Mudavadi na mwanasheria mkuu wa serikali Justine Muturi.

mawaziri hao wanaanza majukumu yao Rasmi baada ya majina yao kuchapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali hapo jana.

BY EDITORIAL DESK