HabariNews

Taasisi ya wahandisi nchini (IEK) imeunga mkono mswada unaoshinikiza upanzi wa miti.

Taasisi ya wahandisi nchini (IEK) imeunga mkono mswada unaoshinikiza upanzi wa miti katika sehemu za ujenzi wa majumba na barabara ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Naibu Mwenyekiti wa kamati ya wanawake wahandisi katika taasisi hiyo Mhandisi Christine Adongo ameshinikiza utekelezaji wa mswada huo kama njia moja ya kupambana na majanga kama ukame.

Mswada huo uliwasilishwa na mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie ukiwataka wanakandarasi kupanda miti katika sehemu zitakazoathirika na shughuli za ujenzi wa barabara.

Kwa upande wake mbunge wa Rangwe kutoka kaunti ya Homabay Lilian Gogo amewataka wanawake wahandisi kujitosa katika ulingo wa siasa.

Kauli ya mbunge huyo inajiri kufuatia ongezeko la idadi ya wanawake waliosomea taaluma ya uhandisi yenye idadi kubwa ya wanaume nchini.

BY EDITORIAL DESK