HabariNews

Mdahalo wa ni nani anayefaa kurithi ardhi ya base titanium waibuka.

Kumeibuka mdahalo wa ni nani anayefaa kurithi ardhi iliyokuwa ikichimbwa madini na kampuni ya basetitanium itakapofunga virago vyake mwaka 2024 katika kaunti ya Kwale .

Baadhi ya wakaazi wakitaka serikali kuchukua ardhi hio kwa uekezaji ama ijenge kambi ya vitengo mbalimbali vya usalama kama njiamojawapo ya kukabiliana na mzozo wa umiliki ambao huenda ukaibuka miongoni mwa wenyeji.

Mashirika ya kijamii ya kutetea haki za kibinadaam yakitaka ardhi hio irudishiwe wakaazi kwani hawajafaidika kikamilifu na faida za madini.

BY EDITORIAL DESK