HabariNews

Salim Mvurya azindua rasmi ujenzi wa taasisi ya kufunza maswala ya bahari na uchumi samawati.

Waziri wa madini na maswala ya Baharini na uchumi sawamati Salim Mvurya amezindua rasmi ujenzi wa taasisi ya kufunza maswala ya bahari na uchumi samawati katika kaunti ya Kwale.

Akizungumza katika uzinduzi wa chuo hicho eneo la Kombani, Mvurya amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho utagharimu shillingi billioni 1.2 .

Aidha tayari millioni 806 zimetolewa Kwa ujenzi wa awamu ya kwanza wa chuo hicho.

Ujenzi huo ukichukuwa takriban miezi 18 kukamilika katika ardhi ya ekari 40.

Kwa upande wake gavana wa Kwale Fatuma Achani ametaka wakaazi kuhusishwa kikamilifu katika mradi huo Kwa kuwapa ajira.

Akisema kuwa anatarajia mradi huo utawanufaisha wenyeji Kwa kiasi kubwa.

BY EDITORIAL DESK