HabariNews

Muungano wa wahudumu wa utalii kaunti ya Kwale umeitaka serikali ya kaunti hiyo kuchimba mabwawa.

Muungano wa wahudumu wa utalii kaunti ya Kwale umeitaka serikali ya kaunti hiyo kuchimba mabwawa katika eneo la Nyango huko Kinango ili kukabiliana na tatizo la baa la njaa.

Mwenyekiti wa muungano huo John Baya amesema kuwa mabwawa hayo ndio suluhu ya kudumu kwa tatizo la ukosefu wa maji na chakula katika eneo hilo.

Akizungumza katika hafla ya ugavi wa chakula cha msaada kwa wakaazi wa eneo hilo, Baya amesema kuwa mradi huo wa maji utaimarisha kilimo kupitia unyunyuziaji mimea.

Kwa upande wake naibu msaidizi wa kamishna katika eneo la Ndavaya Charles Msila amewapongeza wahisani kwa kutoa msaada huo.

Msila amewata wahisani hao kuzidi kuwasaidia waathiriwa wa baa la njaa baada ya eneo hilo kuathirika na janga la ukame.

BY EDITORIAL DESK