HabariNews

Wanawake na vijana kutoka eneo bunge la ShimbaHills wameshinikizwa kupigania nafasi za chifu na naibu chifu.

Wanawake na vijana kutoka eneo bunge la ShimbaHills wameshinikizwa kupigania nafasi za chifu na naibu chifu pindi tu kutakapo ongezwa idadi ya wilaya na lokesheni.

Shinikizo hilo limetoka kwa naibu kamishna wa eneo bunge hilo Moses Karwigi akisema kuwa katika eneo bunge hilo hakuna wanamke katika wadhfa wa chifu wala naibu chifu jambo lililomfanya kuwahamasisha jamii kujitokeza na kupigania nafasi hizo.

Akizungumza eneo la Kizibe wadi ya Mkongani afisaa huyo amewataka wanawake kuondoa uoga dhidi ya nyadhfa hizo.

Wakati huo uo naibu huyo wa kamishna amedokeza kuwa kupitia gazeti la serikali kumeongezwa lokesheni 2 na sub-lokesheni 4 ambapo kunatarajiwa kuwa na nafasi za ajiri ili kuweza kuwasimamia wananchi katika maeneo yao.

BY EDITORIAL TEAM