AfyaHabariNews

Chanjo ya Corona kutolewa katika sehemu za ibada.

Baraza la muungano wa viongozi wa kidini nchini (IRCK) kaunti ya Kwale likishirikiana na wizara ya afya linalenga kuanzisha mpango wa kutoa chanjo ya corona katika sehemu za ibada.

Meneja wa mipango katika baraza hilo Linus Nthigai amesema kuwa wanapanga kutoa chanjo hiyo kwa waumini wao baada ya shamrashamra za sikukuu ya krismasi na mwaka huu.

Akizungumza katika eneo la Diani, Nthigai amesema kwamba viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo watawahamasisha wakaazi kuhusu umuhimu wa kudungwa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Kwa upande wake muuguzi msimamizi katika hospitali ya Diani Grace Thumbi amedokeza kuwa wanalenga kuafikia asilimia 90 ya wakaazi.

Thumbi ameahidi kushirikiana na viongozi hao wa kidini ili kufanikisha shughuli ya utoaji wa chanjo katika kaunti hiyo.

BY EDITOROIAL TEAM