Uncategorized

Mawaziri katika kaunti ya Lamu watafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili.

Mawaziri katika kaunti ya Lamu watafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili na wataweza kupoteza kazi zao wakati wanapofeli kuwahudumia wananchi.

Hii ni kauli ya gavana wa kaunti hiyo Issa Timamy wakati wa kuapishwa kwa mawaziri saba, hafla iliyofanyika katika eneo la Mkunguni mjini Lamu ambapo amesema lazima mawaziri hao pamoja na maafisa wakuu wa idara mbalimbali wawajibike.

Timamy amesema amechukua hatua ya kuwaandika kazi kwa mkataba wa miaka miwili kutokana na kile alichojifunza wakati wa kipindi chake cha kwanza ambapo baadhi ya mawaziri hawakuwa wachapa kazi.

Hata hivyo amemtaka waziri wa Afya Mbarak Mohamed kutatua kilio cha ukosefu wa dawa katika hospitali za umma na vile vile kuonya kupotea kwa dawa hizo.

BY EDITORIAL DESK