BurudaniEntertainmentHabariWorld

MFAHAMU JYGGA LO MSANII WA TANZANIA ANAYEFANANA NA JAY Z

Ramadhan Ali Alawi almaarufu Jygga Lo ni msanii wa mziki wa HipHop  kutoka nchini Tanzania anayezidi kujizolea umaarufu katika Tasnia ya Mziki sio kwa kuimba tu bali pia kutokana na muonekano wake unaoshabiana na ule wa Rapper mkongwe na mkubwa Duniani kutoka Marekani Shawn Corey Carter Almaarufu Jay Z. Mfanano wake na Jay Z mbali na kufanikisha safari yake ya mziki pia umempa manufaa mbali mbali ikiwemo kushinda Tuzo za “Celebrity look alike” 2016 zilizoandaliwa jijini Dar es salam.

Jygga Lo ni kama Mfanano wake na Jay Z unampandisha Bei Na ameweza kufanya Kazi kadha na wasanii wakubwa wa HipHop Bongo akiwemo Baghdad, P Mawenge na Becka Title,

Baada ya kufanya vizuri kwenye ngoma zilizopita Jygga Lo amerudi tena upya na ngoma inayoitwa Burgain Bei chini ya Producer Kondo wa Kori Productions Kutoka Hapa Mombasa.

Isikilize hapa……………….