HabariKimataifaLifestyle

MWANADOA KUFUNGWA JELA MWAKA MMOJA KWA KUCHEPUKA…….!!

Bunge la Indonesia linatarajiwa kupitisha sheria ya uhalifu mwezi huu itakayowaadhibu watu wanaoshiriki ngono nje ya ndoa kwa kifungo cha hadi mwaka mmoja.Mwanasiasa nchini humo -Bambang Wuryanto, ambaye alihusika katika utungaji wa sheria hiyo, alisema kuwa inaweza kuidhinishwa kabla ya mwezi huu kuisha. Iwapo sheria hiyo itapitishwa, itawaadhibu raia wa Indonesia pamoja na raia wa kigeni. Adhabu hiyo ya uasherati inaweza kutekelezwa tu iwapo kuna watu watakaowasilisha malalamiko kwa mamlaka.

Kwa upande wa wanandoa mmoja wao ana haki ya kuwasilisha malalamiko kama mshitakiwa ni mume au mke. Sheria hiyo pia inawaruhusu wazazi wa watu ambao hawajaolewa kuwaripoti kwa kufanya ngono.

Kuishi kama mume na mke kabla ya ndoa pia kutapigwa marufuku na wale watakaopatikana na hatia wanaweza kukabiliwa na hukumu ya kifungo cha miezi sita jela.