HabariNews

Dorcas Ndunga kutoka shule ya shule ya Mekaela Academies Kwale apata alama 419.

Mwanafunzi ambaye anaongoza katika mtihani wa KCPE kaunti ya Kwale ni Dorcas Ndunga kutoka shule ya shule ya Mekaela Academies,kwa kupata alama 419.

Jason Wandera kutoka shule ya Bethany Academy amepata alama 417 huku akifuatwa kwa karibu na Derrick Wamwandu na Titus Lwambi waliopata alama 416 kutoka shule hiyo.

Kwa mara nyengine shule ya msingi ya Masimbani kutoka eneo la Lungalunga imekuwa kifua mbele kwa kupata mwanafunzi bora wa alama 413 huku wanafunzi 25 wakipata zaidi ya alama 400.

John Kanga ni mwalimu mkuu wa shule hiyo.

BY NEWS DESK