Uncategorized

Msako dhidi ya magenge ya vijana waendelea katika kaunti ya kwale.

Idara ya usalama katika kaunti ya Kwale inaendelea kufanya msako dhidi ya magenge ya vijana ambayo yamekuwa yakitekeleza visa vya uhalifu hasa nyakati za usiku.

Kamishna wa kaunti hiyo Gideon Oyagi amesema kuwa baadhi ya vijana wanaosakwa na polisi kwa kujihusisha na magenge hayo ni watoto wa kati ya umri wa miaka 12-17.

Akizungumza na wanahabari mjini Kwale, Oyagi amewalaumu pakubwa wazazi kwa madai ya kutowajibika ipasavyo katika majukumu yao ya kuwalea watoto.

Hata hivyo, kamishna huyo amewahimiza wazazi kaunti hiyo kuwachunga watoto wao wakati huu wanapokuwa nyumbani kwa msimu wa likizo.

Amewataka wazazi kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya wanao ili kuwaepusha dhidi ya kujiingiza katika makundi ya kihalifu.

BY EDITORIAL TEAM