HabariNews

Wakaazi wa Mararani watakiwa kutotegemea chakula cha msaada pekee.

WAKAAZI KATIKA KIJIJI CHA MARARANI ENEO BUNGE LA LAMU MASHARIKI WAMETAKIWA KUTOTEGEMEA CHAKULA CHA MSAADA NA BADALA YAKE KUENDELEZA UKULIMA.

Wakaazi huko Boni katika kijiji cha Mararani eneo bunge la Lamu Mashariki wametakiwa kutotegemea chakula cha msaada na badala yake kuendeleza ukulima.

Kwa mujibu wa mbunge wa eneo hilo Ruweida Mohamed, tabia ya wakaazi kutegemea chakula cha msaada sio jambo la kutegemewa ikiwa wafadhili watajiondoa.

Amewataka wakaazi kutumia maji ya mto uliokaribu kuanza unyunyiziaji wa maji mimea yao.

Vile vile mbunge huyo amewahimiza wazazi kuwasomesha watoto wao akisema ndio njia ya kipekee ya kuepukana na matatizo yanayoikabili jamii hiyo.

BY EDITORIAL DESK