HabariNews

JAMII YAHIMIZWA KUTOWATENGA WALEMAVU WA TAWAHUDI (AUTISM)

Ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha siku ya ulemavu wa tawahudi tarehe 2
Aprili, jamii imehimizwa kutowatenga au kuwabagua watu wenye ulemavu wa
tawahudi ili kuwasaidia katika mustakabali wa maisha yao.

Tawahudi ama Autism kwa lugha ya kiingereza ni ulemavu unaomsababisha
muathiriwa kujirudia rudia, kuwa na matatizo ya mawasiliano, kujitenga
na watu miongoni mwa mambo mengine, ulemavu ambao mtu huzaliwa nao. Watu
wengi katika jamii wakikosa ufahamu kuhusu ulemavu huu.

Mkurugenzi wa baraza la kitaifa kwa watu wenye ulemavu Mathius Mwatsuma
Tsuma, anasema kutokana na hulka yao ya kujitenga na watu imepelekea
wengi kukosa kufahamu kuwa wanahitaji msaada, huku akieleza kuwa
maadhimisho hayo awamu ya nne yatakayofanyika tarehe 2 Aprili, yanalenga
kuchanga fedha zitakazotumika kununua vifaa vya matibabu ya walemavu wa
tawahudi.

Mwatsuma, amesema mikakati inaendelea kuwekwa kuhakikisha kuwa watu
wenye uatilifu wa aina hii wanasajiliwa ili kuweza kunufaika na misaada
na miradi ya maendeleo kutoka kwa serikali.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kutowatenga wala kuwabagua na kuzitaka
familia zinazoishi na watu wenye uatilifu huu kutafuta usaidizi katika
vituo vya afya.

BY ERICKSON KADZEHA.