HabariNews

SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI KUPANUA MAENEO YA KUENDELEZA KILIMO NYUNYIZI ILI KUKABILIANA NA BAA LA NJAA.

Serikali ya kaunti ya Kilifi imesema inaendeleza mikakati ya kupanua maeneo ya kilimo nyunyizi ili kufikia ekari zaidi ya elfu moja kukabiliana na tatizo la baa la njaa ambalo limekuwa likishuhudiwa kila uchao katika kaunti hiyo.


Kwa takriban muongo mmoja sasa wakulima kaunti ya Kilifi wamekuwa wakikosa mavuno mashambani mwao kutokana na ukosefu wa mvua ya kutosha ili kufanikisha kilimo wanachoshiriki.

 
Katibu katika idara ya kilimo kaunti ya Kilifi Teddy Yawa anasema kaunti ya kilifi imekuwa ikipokea mvua isiyozidi mililita 450, hali inayopelekea kukosekana kwa mavuno kwa wakulima.
 

Amesema, mikakati ya kupanua maeneo ya kuendeleza kilimo nyunyizi inaendelea kwenye mto Sabaki na Jaribuni pamoja na kuchimba visima vidogo vidogo vya kuhifadhi maji ili kuendeleza kilimo nyunyizi mbinu anayosema itakabiliana vyema na uhaba wa mvua kwa wakulima.

Hata hivyo anasema mpango wa kilimo nyunyizi umekumbwa na changamoto kufuatia miundo msingi kusombwa na maji kila wakati kunaponyesha.
 

Ametaja kilimo nyunyizi kukosa kukumbatiwa na wakulima wengi kaunti ya Kilifi kufuatia gharama za juu za kununua mafuta yanayotumiwa na mashine za kusukuma maji, huku akieleza kuwa sasa hivi wanaendelea kuhamasisha wakulima kutumia kawi ya jua.

BY ERICKSON KADZEHA