HabariNews

Serikali ya kitaifa yatakiwa kuruhusu ndege za kimataifa kutua katika uwanja wa ndege wa Mombasa.

Serikali ya kaunti ya Kwale sasa inaitaka serikali ya kitaifa kuruhusu ndege za kimataifa kutua katika uwanja wa ndege wa Mombasa ili kuimarisha sekta ya utalii katika eneo la Pwani.

Waziri wa utalii wa kaunti hiyo Michael Mutua amelitaka shirika la ndege ya uturuki kuruhusiwa kutua katika uwanja huo ili kuwavutia wageni zaidi katika kaunti ya Kwale na Pwani kwa jumla.
Akizungumza huko mjini Kwale, Mutua ameahidi kushirikiana na washikadau mbali mbali pamoja na waekezaji ili kutatua changamoto za utalii sawia na kuboresha vivutio vya kitalii.
Mutua ameyasema hayo baada ya kuapishwa kama waziri wa utalii huku Karuwa Tsiwezi akiapishwa kama waziri wa utawala na huduma za umma.
Kwa upande wake gavana wa Kwale Fatuma Achani amewataka mawaziri hao kuwahudumia wakaazi kwa kutatua changamoto zinazoathiri kaunti hiyo.
BY EDITORIAL DESK