HabariNews

Raila odinga aunga mkono ugavi wa mapato kwa kuzingatia idadi ya watu

Kinara wa Azimo Raila Odinga amejitosa rasmi kwenye mjadala kuhusu mfumo wa ugavi wa mapato kwa kuzingatia idadi ya watu One-man-one-vote-one-shilling

Akizungumza katika jumba la Chungwa jijini Nairobi baada ya kukutana na waandalizi wa kongamao la Limuru III, Odinga ameunga mkono mfumo huo ambao umekuwa gumzo kwenye siku za hivi majuzi.

Mjadala huo huenda ukachkuwa mkondo tofauti hapa nchini hasa kufuatia hatua ya viongozi wenye ushawishi mkubwa kujotosa kwenye mjadala huo na kuupigia debe.

Kulingana na Odinga, mfumo ndio mwelekeo pekee unaofaa utakaohakikisha kuna usawa wa maendeleo  na ugavi wa mapato unaostahiki kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

Odinga alibainisha kuwa kumekuwa na taarifa za kupotosha kuhusu mfumo huo ambao sasa unaonekana ni njia ya kubagua maeneo yenye idadi ndogo ya watu.

“This thing has been misrepresented as if it is discriminating against the party of our country, nothing could further from the truth. It is not a question of discrimination. We want to ensure that each and every Kenyan get a fair share…. It cannot be right that some children should get more money as for bursary than other children in other part of the country,” Alisema Odinga.

Ili kufanikisha mjdala kuhusu suala hilo, Odinga ametoa changamoto kwa viongozi kukoma kutumia majukwaa ya kisiasa kuutia dosari mfumo huo.

Alidai kwamba kuna haja kuandaliwa kwa mjadala komavu na uwazi utakaowahusisha wadau mbalimbali ikiwemo wakenya, viongozi na wataalamu ili kujadili kwa kina nafasi na umuhimu wa mfumo huo.

“And I think this is a conversation if we have it openly, open dialogue we will be able to convince majority of the people that this is the right way to go.” Alieleza Odinga.

Awali mjadala huo ulianza baada ya naibu war ais Rigadhi Gachagua kutangaza hadhrani kwamba anunga mkono mfumo huo na kuahidi kuwashinikiza viongozi wengine kuunnga mkono hoja hiyo.

Pia unawezasoma;

BY MAHMOOD MWANDUKA