HabariNews

Gavana wa Kericho Abanduliwa Uongozini

Gavana wa Kericho Eric Mutai amebaduliwa madarakani na Bunge la kaunti hiyo, baada ya Wawakilishi wadi 31 kupiga kura kuunga mkono hoja ya kumwomdoa.

Gavana huyo ameng’atuliwa kutokana na madai ya ukiukaji mkubwa wa katiba, matumizi mabaya ya ofisi na ufujaji wa rasilimali za umma. Hoja hiyo ya kumbandua imewasilishwa na Mwakilishi Wadi ya Sigowet Kiprotich Rogony.

Awali bunge limetarajia gavana Mutai kuhudhuria ili kujitetea dhidi ya mashtaka haayo mazito, lakini hakuwepo na badala yake alituma timu ya wanasheria ikiongozwa na Katwa Kigen. Mutai amedai kuwa amri ya mahakama ya kusimamisha mchakato huo lakini amri hiyo haikuwasilishwa kwa wakati hivyo hoja
iliendelea ilivyopangwa.

Rogony amemshutumu gavana Mutai kwa makosa kadhaa yakiwemo kuongoza kundi la watu kuvamia ardhi ya kibinafsi Kericho ili kuitumia kama jaa la taka lisilokubalika pamoja na kuwashinikiza wanawake kushiriki vitendo vya ngono visivyofaa. Hatima ya gavana sasa ipo mikononi mwa seneti ambapo Spika wa bunge la kaunti hiyo, Dkt. Patrick Mutai anatarajiwa kuandika barua kuwajulisha kuhusu kung’atuliwa kwa gavana huyo.

BY NEWS DESK