MichezoSports

Rodri Mchezaji Bora Ulaya; Ashinda Tuzo ya Ballon D’OR 2024

Mchezaji wa Kiungo cha Kati wa Manchester City na Spain Rodri ndiye Mshindi wa Tuzo ya Ballon D’or mwaka 2024.

Rodri ameshinda Tuzo hiyo makala ya 68 kwa kuwapiku Vinicius Junior na Jude Belingham wa Real Madrid, waliomaliza nafasi ya 2 na 3 mtawalia.

Katika sherehe zilizofanyika usiku wa Jumatatu Rodrigo maarufu Rodri amekuwa na msimu mzuri 2023/24 kwa kuisaidia Klabu yake ya Man City kushinda ubingwa wa ligi Kuu ya Uingereza, Kombe la UEFA super Cup, na vile vile alishinda Ubingwa wa UEFA Euro 2024.

Anakuwa mchezaji wa haiba ya aina yake katika safu ya Kiungo cha kati Mkabaji kushinda Tuzo hilo lililotawaliwa na Washambuliaji kwa muda mrefu.

Mara ya mwisho kiungo cha kati kushinda Tuzo hilo alikuwa ni Mkroeshia Luca Modric mwaka wa 2018.

Katika Tuzo hizo aidha Kinda wa Barcelona na Uhispania umri wa miaka 17, Lamine Yamal aliibuka na Tuzo Bora ya dhahabu kwa upande wa vijana maarufu Kopa Trophy.

Naye Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti akiibuka kuwa Mkufunzi Bora upande wa wanaume msimu wa mwaka 2023-2024.

By Mjomba Rashid