Habari

KIKUNDI CHA SAUTI YA WAZEE KAUNTI YA KILIFI CHATOA SAUTI KUHUSU CHANJO YA CORONA

Kikundi cha Sauti ya Wazee kaunti ya Kilifi kinaitaka serikali kuwa makini wakati chanjo ya ugonjwa wa Corona itakapofika nchini.

Wakiongozwa na katibu mkuu wa kikundi hicho Simon Mvondi wanasema huenda chanjo hiyo ikawa na madhara mengi kwa wakaazi nchini akisema inafaa kutolewa kwa hiyari.

Mvondi vile vile ameitaka serikali kusambaza nakala za ripoti ya BBI kwa wakenya wote kabla ya hoja hiyo kufika kwa wananchi.

Wakati uohuo wameitaka serikali kuwanusuru wazee eneo la pwani wakisema kwa sasa idadi kubwa ya wazee wanauwawa kinyama kwa madai ya uchawi.

Wanasema wengi wao hulazimika kuhama makaazi yao kutokana na hofu ya kuvamiwa na kuuwawa kinyama wakiwashutumu vijana kuwa msitari wa mbele kutekeleza mauwaji hayo.

Haya yanajiri huku mzee mmoja akiuwawa kinyama huko Adu eneo bunge la Magarini.

Joseph yeri.

 

Comment here