HabariSiasa

Wito umetolewa kwa wakaazi kaunti ya Kilifi pamoja na Pwani kwa jumla kuungana na kuingia chama cha pwani ili kufanikisha malengo yao.

Kulingana na kinara wa KADU ASILI Gerald Thoya wakati umefika kwa viongozi kutoka ukanda huo kuongoza wakaazi kupitia kwa chama hicho kwa manufaa ya wenyeji.

Thoya anasema chama hicho kwa sasa kiko imara baada ya jaribio la mapenduzi linalodaiwa kuongozwa na baadhi ya wabunge eneo hilo kutibuka.

Kinara huyo amesistiza kuwa wenyeji wote eneo hilo wako huru kujiunga na chama hicho akisema sharti kanuni za chama hicho zifuatwe.

Anasema ipo haja ya maeneo mengi eneo hilo kubadilisha uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao ili kuimarisha maisha ya wenyeji.

Mapema mwaka huu wajumbe kadhaa kaunti ya Kilifi wanaomuunga mkono naibu rais William Ruto wanadaiwa kutekeleza mapenduzi katika chama hicho kabla ya uongozi kuelekea mahakamani na kupata ajizo la mahakama.