HabariNews

Shirika la msalaba mwekundu lalenga kuanzisha mpango wa kuwanunua na kuwachinja mifugo.

Shirika la msalaba mwekundu linalenga kuanzisha mpango wa kuwanunua na kuwachinja mifugo walioathirika na makali ya janga la ukame katika kaunti ya Kwale.

Mshirikishi wa shirika hilo kaunti ya Kwale Mohammed Mwaenzi amesema kuwa wanalenga kuwanunua mifugo 500 walioathirika na ukame katika kaunti hiyo.

Mwaenzi amesema kwamba mpango huo unalenga kuhakikisha wakaazi hawapati hasara ya mifugo wao wanaofariki kutokana na ukosefu wa maji na lishe.

Ni mpango ulioungwa mkono na gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya aliyewataka wakaazi kuwauza mifugo wao ili wasipate hasara.

Haya yanajiri huku tayari zaidi ya mifugo elfu 3 wakiripotiwa kufariki katika kaunti ya Kwale.

BY NEWS DESK.