HabariNews

Zaidi ya walimu 900 wa shule za chekechea (ECDE) wameajiriwa na serikali ya kaunti ya Kwale.

Zaidi ya walimu 900 wa shule za chekechea (ECDE) wameajiriwa na serikali ya kaunti ya Kwale kama njia mojawapo ya kukabiliana na uhaba wa walimu.
Gavana wa Kwale Salim Mvurya amedokeza kwamba baadhi ya walimu hao wamepelekwa katika shule zaidi ya 500 za chekechea zilizojengwa na serikali ya kaunti.
Wakati huo huo, Mvurya amesema fedha zaidi zitatengwa katika bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2021/2022 za kuwaajiri walimu zaidi katika shule hizo ili kukabiliana na uhaba wa walimu kaunti hiyo.