GadgetsHabariMazingiraNews

MSHIRIKISHI MKUU NEMA KAUNTI YA MOMBASA SAMUEL LOPOKOIT AMESEMA BIDHAA ZA PLASTIKI ZINAZOSHUHUDIWA NCHINI ZIMETOKA MATAIFA JIRANI.

Uwepo wa bidhaa za plastiki bado unaendelea kutumika hapa nchini hata baada ya kupigwa marufuku kwa muda sasa.

Kulingana na mshirikishi mkuu wa Shirika la mazingira la NEMA kaunti ya Mombasa Samuel Lopokoit, wingi wa plastiki zinazoshuhudiwa zinatoka katika nchi jirani na wafanyibiashara.

Lopokoit amesema asilimia themanini pekee ndio iliyoweza kufikiwa katika kukabiliana na matumizi dhidi ya plastiki.

Aidha amesema kwamba kwa sasa wanataka kubuni mbinu za kukabiliana na chupa za plastiki zinazouziwa maji na akiongeza kuwa baadhi ya bidhaa ni vigumu kuhifadhiwa bila plastic kwa sababu za kiafya na wanataka kubuni mbinu maalum za kuweza kutumia plastiki kwa njia nyingine.