HabariNews

Kuadhimisha siku ya wanawake kwale.

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wanawake duniani mashirika ya kutetea haki za kibaadamu kaunti ya Kwale yanasema kuwa kukosekana kwa Sheria ya kuwalindana waathiriwa wa dhulma za kijinsia kumekuwa kizingiti katika vita dhidi ya dhulma hizo.
Afisaa wa mipango kutoka shirika la kijamii la NETWORK FOR ADOLESCENT AND YOUTH OF AFRICA( NAYA) Dorcas Mwachi amesema kuwa kuna haja ya Sheria kuundwa ya kuwalinda waathiriwa wa dhulma za kijinsia kama njia ya kupigania haki za wananchi.
Aidha M amesema kuwa ipo haja ya viongozi hususan wananwake walio katika nyadhifa za uongozi kuhakikisha kuwa mswada huo unapitishwa ili kukomesha dhulma za kijinsia.
kauli yake iliungwa mkono na mratibu wa tume ya kitaifa ya ardhi kaunti ya Kilifi Ummi Kugula akisema kuwa japo wanawake wameanza kutambulika lakini mila na desturi zimesalia kuwa chanzo kikuu cha dhulma miongoni mwa jamii hivyo ameitaka serikali kuingilia kati.

>>news desk