HabariNews

Mwanamume mwenye umri wa miaka 30 anazuiliwa katika kituo cha polisi kisiwani Amu kwa madai ya mauaji.

Mwanamume mwenye umri wa miaka 30 anazuiliwa katika kituo cha polisi kisiwani Amu kwa madai ya mauaji.
Mshukiwa anadaiwa kumuua mwenzake wa umri 21 kwa kumdunga kisu shingoni baada ya tofauti kutokea kati yao kuhusu masuala ya siasa.
Kulingana na kinara wa polisi kaunti ndogo ya Lamu ya Kati Geoffrey Osanan, kisa hicho kimetokea katika kijiji cha Wiyoni ambapo mshukiwa aliweza kutoroka lakini baadae akakamatwa kupitia ushirikiano na wananchi.
INSERT: OCPD MAUAJI.
Baadhi ya familia ya mwendazake wakiongozwa na Walid Ahmed, wameitaka serikali kuchunguza kisa hicho na kuhakikisha haki imetendeka.