HabariMombasaNews

Zaidi ya familia 1,000 eneo bunge la Changamwe kunufaika na bima ya kitaifa ya matibabu NHIF.

Zaidi ya familia 1,500 kutoka eneo bunge la Changamwe kaunti ya Mombasa zinatazamiwa kunufaika na bima ya kitaifa ya matibabu NHIF.
Mpango huu ni mojawapo ya mikakati ya kuhakikisha mpango wa afya bora kwa wote uliozinduliwa na rais Uhuru Kenyatta mwezi Februari eneo bunge hilo unaafikiwa pamoja na kuimarisha sekta ya afya.
Wakaazi wa eneo hilo wamesema bima ya NHIF imewasaidia wengi kupokea huduma za matibabu kinyume na awali ambapo baadhi ya wakaazi walitaabika kufikia matibabu kutokana na gharama ya juu.