Maseneta nchini wameanzisha uchunguzi kuhusiana na utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na idara ya utabiri wa hali ya hewa kwa madai kuwa ni usioaminika.
Watungaji sheria hao wameanzisha uchunguzi huo kubaini iwapo utabiri unaotolewa na idara ya hewa ni matokeo ya matumizi ya teknolojia ya kizamani
Kamati ya mali ya umma imeitaka idara hiyo kufafanua aina wa vifaa vinavyotumika kunasa taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya utabiri na muda ambao vimekuwa vikitumika.