HabariMombasaNews

IDARA YA USALAMA YATAKIWAKUZIFUNGA MASKANI 8 ZA BIASHARA YA VILEO HARAMU.

Wakaazi wa eneo la tiwi kaunti ya kwale wanaitaka idara ya usalama kuzifunga maskani 8 zinazotumika kuendeleza biashara ya vileo haramu katika eneo hilo.
Wakiongozwa na Baby Hamisi wanasema kuwa maeneo hayo yamechochea pakubwa kudorora pakubwa kwa usalama kwani magenge ya kihalifu hutumia maskani hizo kama maficho yao.
Wameishtum idara ya polisi wakiitaja kama yenye kuchangia ongezeko la visa vya uhalifu kwa kukosa kuwakabili wahalifu wanaowasilishwa kwao.
Hata idara ya usalama ikiongozwa na naibu kamishna eneo la matuga Lucy Ndemo ameitaka jamii kutowaficha vijana wanaojihusisha na uhalifu ili sheria ichukue mkondo wake.

BY EDITORIAL TEAM