HabariMombasaSiasa

MWANIAJI UGAVANA MOMBASA KWA TIKETI YA UDA HASSAN OMAR SARAI AIDHINISHWA NA IEBC KUWANIA UGAVANA.

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imemuidhinisha rasmi Mwaniaji Ugavana Mombasa kupitia chama cha UDA Hassan Sarai na Mgombea Mwenza wake Selina Maitha.
Akizungumza baada ya kuidhinishwa, Sarai amesema uchaguzi wa sasa ni muhimu kwa wakaazi wa Mombasa kwa kuwa unanuiwa kuwakomboa kutokana na viongozi wafisadi.
Sarai amesema baadhi ya viongozi wamekosa maadili na wamekuwa wakiendesha uongozi mbaya kwa wakaazi wa Mombasa.
Mgombea Huyo amewaahidi wakaazi wa Mombasa kuwa uongozi wao utarejesha huduma za bandari ya Mombasa -KPA na vile vile kuwachukilia hatua za kisheria waliochagania huduma hizo kuhamishwa hadi Naivasha.

>>news desk.