HabariMazingiraSiasa

Wanaharakati wa mazingira wazindua kampeni ya kupanda miche milioni moja.

Wanaharakati wa mazingira kaunti za Lamu, Nairobi na Nakuru wamezindua kampeni ya kupanda miche milioni moja katika kaunti ya Lamu.
Kampeni hiyo imepewa jina “One Million Trees For Teddy” imezinduliwa kwa heshima ya kumuenzi mjukuu wa Dedan Kimathi alieaga dunia mwezi uliopita huko Lamu katika zoezi la kupanda Miti eneo la Mpeketoni na Witu.
Kampeni hiyo inaongozwa na mkurugenzi mtendaji wa Dedan Kimathi Foundation- Evelyn Wanjugu na kufikia sasa wanamazingira hao wamepanda miche elfu thelathini na wanalenga kupanda miche milioni thelathini huko Lamu chini ya muda wa miaka miwili.
Aitha, Wanjugu amesema kuwa Dedan Kimathi Foundation itaendelea kupanda miche kote nchini ili kuyatunza mazingira yetu.

>> News Desk…