HabariMazingira

Mashirika ya kijamii ukanda wa Pwani yazidi kuendesha kampeni ya kupanda mikoko .

Mashirika ya kijamii ukanda wa pwani yanaendesha kampeni ya kupanda mikoko 325, 000 ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kuinua uchumi wa eneo hilo.
Shirika la Rotary club pamoja na For Trees Club yanaendesha kampeni hiyo katika kaunti za Kwale na Kilifi, Zoezi ambalo linalenga kupanda mikoko milioni moja kwenye ukanda wa pwani kufikia mwishoni mwa huu.
Kwa mujibu wa rais wa Rotary Club Malindi Conrad Masinde, kufikia sasa wamepanda mikoko elfu mia moja kwenye kisiwa cha Kirepwe kule Watamu na zaidi ya elfu mia mbili katika eneo la Ganze kaunti ya Kilifi.

>> News Desk…