Habari

Taasisi ya watoto wanaoishi na ulemavu yaitaka serikali kuu kuongeza mgao wa bajeti wa taasisi hio.

Taasisi ya watoto wanaoishi na ulemavu wa kuzungumza, kusikia na kuona nchini imeitaka serikali kuu kuongeza mgao wa bajeti ya taasisi hio ili kuhakikisha watoto walio na mahitaji maalumu wanapata elimu bora.
Kulingana na mwenyekiti wa taasisi hio Francis Ng’ang’a aliyekuwa akizungumza mjini Kwale umetaja ukosefu wa fedha za kutosha kama changamoto kuu inayosababisha vikwazo kwa watoto hao.
Akigusia swala la elimu Ng’ang’a ameelezea masikitiko yake ya kukosekana kwa chuo kikuu cha mafunzo ya watu wanaoishi na walemavu wa kusikia na kuona nchini, akisema watoto wengi husalia kufanya kazi za mikono pindi wanapomaliza kidato cha nne.

>> News Desk…