Habari

Gavana wa kaunti ya Kwale amewataka wazazi kuwa mstari wa mbele kuwaelekeza watoto.

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amewataka wazazi kuwa mstari wa mbele kuwaelekeza watoto wao ipasavyo kutokana na kukithiri kwa visa vya watoto kuwa na maadili potofu. Akizungumza katika bustani ya Baraza mjini Kwale wakati wa sherehe ya kuwatuza wanafunzi sawia na shule zilizofanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa KCPE na KCSE wa mwaka 2021, Mvurya amewataka wazazi kukoma kutumia mitandao ya kijamii wanapokuwa na vikao na watoto wao akisema kuwa imechangia pakubwa watoto kujihisi wametengwa. Mvurya amesema kuwa wazazi wa sasa wamekuwa hawana muda wa kuzungumza na watoto wao hali ambayo imechangia visa vingi vya utovu wa nidhamu. Akigusia swala la basari Mvurya amesema kuwa kutokana na uaminifu uliojengwa na wizara ya elimu nchini, Zaidi ya watoto elfu moja walijiunga na shule za kitaifa mwaka huu kupitia mpango wa elimu ni sasa. Ni kupitia hali hio ambapo mvurya amewarai wakaazi wa Kwale kuwachagua viongozi wanaostahili ili wahakikishe mpango wa kuwasomesha watoto unaendelea.

>> News Desk…