Habari

Shirika la Search for Common Ground limeanzisha mradi wa kuhamasisha jamii.

Shirika la Search for Common Ground limeanzisha mradi wa kuhamasisha jamii kuhusu namna ya kudumisha amani na kusuluhisha na aina zozote za Mizozo, wakati na hata baada ya uchaguzi. Afisa mkuu wa miradi katika shirika hilo Zena Hassan amesema mradi huo uitwao “Uchaguzi Bila Balaa, unahusisha kutoa elimu kwa maafisa wa elimu kwa viongozi mbali mbali ambao watatumika kama watatuzi wa mizozo katika jamii. Zena amesema mradi huo utaendeshwa kwenye kaunti za Mombasa, Kwale, tanariver, Garissa na Lamu na Kilifi. Vile vile amesema mradi huo umefika kwa wakati unaofaa hasa baada ya tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa nchini NCIC kuorodhesha kaunti ya Mombasa miongoni mwa kaunti zenye uwezekano mkubwa wa kushuhudia vurugu wakati wa Uchaguzi mkuu. Wakati huo huo naibu kamishna wa Kaunti eneo la Mariakani Baraza Denis, amesema vyombo vya usalama vimejiandaa vilivyo kuhakikisha vurugu za aina yeyote zinakabiliwa kwa wakati msimu huu wa kampeni za uchaguzi. Vile vile ameonya wanaoeneza propaganda kuwa tayari washindi wa uchaguzi mkuu ujao washajulikana.

>> News Desk…