Habari

IEBC inafanya kikao na wagombea wa urais Agosti 9.

Tume ya uchaguzi nchini IEBC inafanya kikao na wagombea wanne wa urais kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu kujadili matakwa ya wagombea hao.
Muungano wa Azimio uliiandikia IEBC barua wakitaka kujua vituo, sajili na kampuni ya kuchapisha kura.
Kulingana na afisa mkuu mtendaji wa IEBC Marjan Hussein Vifaa vya Kims ambavyo vitatumika wakti wa uchaguzi vina taarifa mbili muhimu ikiwa ni maelezo ya mpiga kura katika vituo maalum vya kupigia kura ambayo ni majina, vituo vya kupigia kura, nambari ya kitambulisho, picha na tarehe ya kuzaliwa.
Marjan ameongezea kuwa mwaka wa 2017 walinunua vifaa vya Kims 45,000 na kufikia sasa vifaa 41,000 viko kwenye hali nzuri ya kutumika katika uchaguzi wa mwaka huu.

>> Editorial Desk…