Habari

USIMAMIZI WA BANDARI YA LAMU KUWEKA MIKAKATI KUONGEZA WAWEKEZAJI.

Usimamizi wa bandari ya Lamu umesema unafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wawekezaji zaidi wanawekeza katika bandari hiyo.
Mkurugenzi mkuu bandarini humo Stephen Ikua amesema shughuli katika bandari hiyo zinaendelea na kwamba wanaendelea kuwavutia wawekezaji zaidi ili kuinua uchumi wa taifa.
Akiongea baada ya kikao na wawekezaji kutoka nchini Qatar, Ikua amesema wanatarajia wawekezaji zaidi kutoka mataifa ya Dubai na Oman.
Kwa upande wake, Mhandisi katika bandari hiyo Vincent Sidai amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa bandari hiyo imekamilika na kwamba jumla ya meli 12 zimeweza kutia nanga na mizigo mbalimbali.
Sidai aidha amesema kuweko kwa wawekezaji zaidi kutazidisha oparesheni katika bandari hiyo na hatimaye kutoa nafasi nyingi za ajira kwa vijana.

>> Editorial Desk…