HabariNewsSiasa

IEBC YAPOKEA SHEHENA YA KWANZA YA KARATASI ZA KUPIGIA KURA.

Tume ya uchaguzi nchini imepokea shehena ya kwanza ya
karatasi za kupigia kura zitakazotumika katika uchaguzi mkuu wa
agosti 9.
Akipokea shehena hiyo katika uwanja wa ndege wa jomo
Kenyatta Jijini Nairobi, mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
amesema kwamba mipango yote ya uagizaji wa karatasi hizo
imekamilika ambapo kwa sasa uchapishaji wake unaendele.
Chebukati amesema hakutakuwa na karatasi zaidi huku akipinga
madai ya kuwepo kwa uchapishaji wa karatsi hizo kinyume na
sheria.
Chebukati vilevile amesema kuwa wataendelea kupokea karatasi
hizo za kupigia kura hadi tarehe 29 mwezi huu wa Julai zile za
urais zikiwa za mwisho
Wakati uo huo Chebukati amewataka wakenya na viongozi
wengine kukoma kuendeleza propaganda ambazo huenda
zikaleta taharuki uchaguzi unapokaribia.

>>>BY MAHMOOD MWANDUKA