HabariNewsSiasa

MIKAKATI YA KUHAKIKISHA KUWA AMANI INADUMISHWA YAENDELEA KUWEKWA KILIFI.

Mikakati ya kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao unakuwa wa
amani inaendelea kuwekwa, huku hali ya utulivu ikiendelea
kushuhudiwa kaunti ya Kilifi.
Kwa mujibu wa naibu kamishna eneo bunge la Kilifi Kaskazini
Geofrey Tanui, kamati za amani zinazowajumuisha wadau mbali
mbali zimeundwa ili kuhakikisha amani inadumishwa, huku vikao
vya kamati hizo vikifanyika kila mwezi.
Tanui hata hivyo ameowanya vijana dhidi ya kutumiwa kuzua
vurugu akieleza kuwa mkono wa sheria utakabiliana na mtu
binafsi.

Kwa upande wake Joseph Sianda afisa wa shirika la kusambaza
amani la KECOSCE, amesema tayari wameanza kutoa mafunzo
kwa wazee wa mitaa 150 kuhusu jinsi ya kufanikisha mikakati ya
kudumisha amani.
Hatua hii ikijiri baada ya shirika la KECOSCE kuwapa mafunzo
maafisa ishirini wa kushughulika kutambua semi za chuki na
uchochezi kaunti hii ya Kilifi.

>>>BY ERICKSON KADZEHA.