HabariKimataifaNews

Shirika la Afya Duniani (WHO) limefahamisha kuwa linatazamia kubadili jina la ugonjwa wa homa ya nyani.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limefahamisha kuwa linatazamia kubadili jina la ugonjwa wa homa ya nyani, na hivyo kuomba usaidizi wa umma wa kupendekeza jina lisilokuwa na unyanyapaa kwa ugonjwa huo unaoenea kwa kasi.

Watu 31,000 wameambukiwa ulimwenguni kote na wengine 12 wamefariki.

Kwa wiki kadhaa, Shirika hilo limekuwa likielezea wasiwasi wake kuhusu jina linalotumiwa kwa ugonjwa huo.

Wataalamu wanaonya kuwa jina hilo linaweza kusababisha vitendo vya unyanyapaa kwa nyani licha ya kuwa na jukumu dogo katika kuenea kwa ugonjwa huo.

Hivi majuzi nchini Brazil, kumeripotiwa vitendo vya watu kuwashambulia tumbili kutokana na hofu ya ugonjwa huo. Virusi hivyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza kwenye nyani waliohifadhiwa kwa ajili ya utafiti nchini Denmark mwaka wa 1958, lakini ugonjwa huo ukagundulika kwa mara ya kwanza kwa binadamu mwaka 1970 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

BY EDITORIAL DESK